Jiunge nasi katika Agritour - Bata Shambani, tukio la kipekee la siku mbili linalolenga kukuza kilimo rafiki kwa mazingira na ustawi wa jamii. Tukio hili linaleta pamoja wakulima, wataalamu wa kilimo, vijana, na watetezi wa mazingira kwa ajili ya kujifunza, kushirikiana, na kufurahia.
Kauli mbiu:
"Linda Mazingira. Lima Kitaalamu. Jifunze kwa Vitendo."
Mbinu za kilimo hai na kilimo mseto
Utunzaji wa udongo na matumizi bora ya maji
Umwagiliaji unaookoa maji na teknolojia rahisi za kilimo
Kutembelea mashamba ya mfano
Kujifunza kwa vitendo kuhusu utunzaji wa mazingira kupitia kilimo
Muziki, michezo ya asili, jioni ya hadithi na moto wa kambi
Usiku wa kusherehekea kilimo na utamaduni
Usafiri wa kwenda na kurudi
Kambi salama na mazingira rafiki kwa washiriki wote
Menyu ya vyakula vya kiasili
Vyakula vinavyopatikana mashambani
Mashindano ya ujuzi wa kilimo
Tuzo kwa washiriki wanaoonyesha ubunifu na maarifa
Reserve your ideal trip early for a hassle-free trip; secure comfort and convenience!